Breaking

Alhamisi, 21 Machi 2019

Happy Brithday Apostle Boniface Mwamposa Bulldozer

Leo Tarehe 21 March ni siku ambayo nina mshukuru Mungu sana kwa kuwa ni kumbukumbu ya siku niliyozaliwa . Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na wazazi wangu maana hakika ilikuwa ni kwa kusudi la Mungu mimi kuzaliwa na kufanyika baraka na msaada katika maisha ya watu wengi ambao nimekuwa nikiwahudumia katika maisha yangu ya Utumishi. 


Hakika nimemuona Mungu akitenda mambo makuu sana katika maisha yangu, na leo nikiwa naadhimisha siku yangu ya kuzaliwa natangaza siku yako ikawe Nuru na Nyota yako ikang'ae sana . Mwezi huu tunatembea na somo USIOGOPE nami ninakwambia USIOGOPE nawe utamuona Mungu akikuinua katika viwango vya juu sana katika mwaka huu wa Upako wa Kufanya Mambo Makuu kwa Njia Rahisi sana. Pokea kuinuliwa, Pokea Nuru katika maisha yako na Nyota yako Ikang'ae sana kwa Jina la Yesu Kristo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni